Menu
COUNTDOWN TO PEACE DAY
Sisi ni kina nani

PEACE ONE DAY NI NINI?

Jeremy Gilley ni mwigizaji aliyegeuka kuwa mtengenezaji filamu, ambaye mwishoni mwa miaka ya 1990 alinza kushughulikia sana maswali kuhusu hali halisi muhimu ya ubinadamu na suala la amani. Aliamua kuchunguza maswali haya kupitia katika mbinu ya filamu, na hususan, kuunda filamu ya hali halisi iliyofuatia kampeni yake ya kuanzisha siku ya kila mwaka ya kusitisha vita na kutokuwa na vurugu.

Mnamo mwaka 1999 Jeremy aliasisi Peace One Day, shirika lisilokuwa la faida, na mnamo mwaka 2001 jitihada za Peace One Day zilituzwa wakati ambapo mataifa ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa pamoja na kwa msisimko mkubwa waliichukua kwa mara ya kwanza siku ya kila mwaka ya kusitisha vita na kutokuwa na ukatili ulimwenguni kote ya Septemba 21- Siku ya Amani.

Lengo la Peace One Day ni kuweza kurasmisha Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21, na kuifanya kuwa siku ambayo itajitosheleza-yenyewe, siku ya kila mwaka ya umoja wa ulimwenguni, siku ya ushirikiani kati ya tamaduni katika kiwango ambacho ubinadamu hawajawai kujua.

Kwa miaka na mikaka, mamilioni ya watu wamekuwa wakijishughulishwa na Siku ya Amani katika kila nchi ya ulimwengu, na mamia ya mashirika yameweza kutekeleza shughuli za kuokoa maisha kwenye maeneo yenye mapigano. Kampeni na shughuli za Peace One Day, katika Elimu, Muziki, Filamu, Michezo, Densi, Sanaa na Mtandaoni zimethibitisha kwamba siku hiyo ni kweli na inasaidia

Akiwa ametiwa moyo na punguzo la 70% lililorekodiwa katika matukio ya vurugu kwenye Siku ya Amani nchini Afghanstan (chanzo: Idara ya Usalama na Amani ya Umoja wa Mataifa), na ili kujenga msingi thabiti wa kwa kufikia 2012, Jeremy alizidua kampeni ya Kusitisha vita Ulimwenguni Kote ambayo ilihususha uundaji wa misururu ya miseto ya Peace One Day, kila moja ikiwa mshiriki mwongozi: Mseto wa shirika lisilokuwa la kiserikali; ‘mseto wa kupunguza vurugu ya nyumbani’; mseto wa wanafunzi; na mtandao wa shule.

Kupitia katika jitihada na ushirikiano wetu sisi wenyewe tukiwa na wahusika mbalimbali, Peace One Day italenga katika kuhimiza mashirika na watu binafsi kuchukua hatua mahususi za kupunguza vurugu kukaribiana na mada: Nani Utaridhiana Naye Amani?

SEPTEMBA 21
Ni Siku ya Amani
Ufahamisho Ulimwenguni
1.5bn
2.2bn
2014
2016

Thamani ya Kuchukua Hatua

Ripoti Ya Siku Ya Amani 2014 Ya Mckinsey & Co:
2.2
Bilioni watu wazi
Yafuatayo ni maelezo ya hivi punde kuhusu ni watu wangapi walikuwa na ufahamu siku hiyo, adhari zake katika vurugu na namna tunavyoweza kuendeleza matokeo haya kwa Siku za Amani za siku zijazo

Milioni WATU UFAHAMU

SEPTEMBA 21
NI SIKU YA AMANI
Ufahamisho wa Siku ya Amani huunda hatua, na hatua hiyo huoka maisha.
Jude Law - Balozi wa Peace One Day