Menu
Elimy & Siku ya Amani

Siku ya Amani ya Septemba 21 inatoa fursa nzuri ya kusherehekea elimu ya amani kwa kuandaa shughuli yako mwenyewe.

Kama ungependa kujiunga na maelfu wanaosherehekea siku hii na unahitaji kutiwa moyo kwa ajili ya sherehe yako ya Siku ya Amani tafadhali tazama baadhi ya sehemu zenye kuvutia kutoka Siku ya Amani ya 2015 au tembelea ukurasa wa kuhusishwa. Na tafadhali usisahau kutujulisha utakachofanya kupitia fomu yetu ya shughuli au kwa kupitia barua pepe

 

Twaweza tukakutolea nini?

Rasilimali ya Elimu ya Amani Ulimwenguni; mipango ya masomo yenye mwingiliano inayochunguza masuala kama vile kupambana na uonevu, utatuzi wa migogoro na uraia wa kimataifa. Imetengenezwa na waelimishaji kwa waelimishaji, lengo la rasilimali zetu ni kuleta mjadala na hatua ya vitendo miongoni mwa mamilioni ya wanafunzi duniani kote.

Mtandao mkubwa wa waelimishaji ulioko katika zaidi ya nchi 140; jukwaa ambalo huleta pamoja zaidi ya shule 9,000 na taasisi za elimu, na hutolea walimu na wanafunzi mawazo ya vitendo kwa ajili ya shughuli ya Siku ya Amani.

Mazungumzo ya Amani; fursa kwa darasa lako kuzungumza moja kwa moja na mwanzilishi wetu, Jeremy Gilley. Kugundua zaidi kuhusu safari ya Siku ya Amani na kushiriki katika mazungumzo kuhusu mawazo yako kwa Siku ya Amani.

Vifaa vya shughuli ya Siku ya Amani; hati rahisi ya mwongozo  wa kukusaidia katika mipango na utekelezaji wa sherehe ya kufana ya Siku ya Amani, pia inatoa mawazo mengi ya  kuwahamasisha vijana wapatanishi kuleta mabadiliko.

Wafuasi
Rasilimali ya elimu ya amani ulimwenguni

Watie moyo na kuwawezesha wanafunzi wako kuweza kutumia maarifa na ujuzi wao kwa jina la amani!

Rasilimali ya bure na yenye utajiri kuhusu vyombo vya habari, inachunguza masuala kama vile ushirikiano wa kitamaduni, utatuzi wa migogoro na jinsi ya kumaliza uonevu, pia zinaonyesha uwezo za michezo, muziki, dansi, sanaa na mchezo wa kuigiza ndani ya mazingira ya amani.

rasilimali zetu za elimu ya amani ulimwenguni zinapatikana katika  Lugha 6 rasmi za Umoja wa Mataifa (Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kimandarini na Kirusi) rasilimali hizi zimepatwa na maelfu ya waelimishaji katika karibu kila nchi ya ulimwengu.

 

Jiunge na tandabui ya shule yetu

Bofya hapa kujiunga na Tandabui ya Shule 'na kuweza kupata huduma ya zana mbalimbali za msaada wa Elimu ya Amani ya Ulimwenguni, pamoja na Rasilimali yetu ya Elimu ya Amani ya Ulimwenguni na miradi mbalimbali inayozingatia sehemu mbalimbali za mtaala, na fursa ya kushirikiana moja kwa moja na shule za kitaifa na kimataifa ili kuwapa wanafunzi wako hisia ya kweli ya ushirikiano wa kitamaduni .

Hapa ni baadhi tu mifano michache ya jinsi wanachama wa Tandabui ya Shule wamesherehekea Siku ya Amani:

 

Mazungumzo ya Amani

Mradi wa mazungumzo yetu ya Amani hutumia Skype ili kumuwezesha Jeremy kuzungumza na wanafunzi katika madarasa duniani kote, kuhamasisha kizazi cha vijana wanaounga mkono Siku ya Amani. Mazungumzo ya Amani yamefanyika kwa wanafunzi katika nchi zaidi ya 50 duniani kote.

Kama ungependa shule yako ishirikishwe katika Mazungumzo ya Amani  tafadhali wasiliana nasi kwa kupitia barua pepe.

Hebu tazama uteuzi wa Mazungumzo ya Amani yaliopita:

Elimu & maeneo ya maziwa makuu ya afrika

kwa ufadhili wa ukarimu wa Taaasisi ya Howard G. Buffett, tumeanzisha bango la Elimu ya Amani ili kuunga mkono kampeni yetu inayolenga ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika.

 

Miradi ya Amani

Mahali palipo na mafunzo yote yanayohusiana na amani 

Amani hutoa sababu kuu ya shughuli za elimu. Eneo hili linashirikisha kuongezeka katika maktaba ya miradi ya kusisimua ya Amani itokayo katika jamii ya mashirika na watu binafsi duniani kote. Miradi hii huzungumzia mambo mbalimbali ya mtaala, hivyo basi kuruhusu elimu ya amani mwaka mzima kuwa chanzo cha wanafunzi kuleta shughuli zao katika siku ya Amani ya kila mwaka,sambamba na mamilioni ya wengine duniani kote. 

Sehemu muhimu ni kama: