Menu
FILAMU BAINISHI YA PEACE ONE DAY

Filamu mbili za kwanza za Jeremy Peace One Day na Siku Baada ya Amani zimechezeshwa ulimwenguni kote na mamilioni ya watu. Siku Baada ya Amani imetayarishwa kwa ushirikiano wa BBC na Passion Pictures. Peace One Day Sehemu ya Tatu (imetayarishwa na Jeremy na Jude Law) na ilirushwa hewani mnamo mwaka wa 2010 kwenye BBC World, na kuweza kufikia familia milioni 306 katika nchi zaidi ya 200.

TAZAMA MTANDAONI

Kama una muda tu wakutazama mojawapo kati ya zile filamu tatu zilizotajwa hapo juu, tunapendekeza Siku Baada ya Amani, ambayo unaweza kutazama bila malipo, mtandaoni hapa.

SIKU BAADA YA AMANI (The Day After Peace)

Hii ni filamu ya hali halisi ya pili ambayo ni ya kutunzwa tuzo kutoka kwake Jeremy Gilley, ambayo inafuatilia kazi yake ya kuonyesha  ulimwenguni kote siku hii ya ksitisha vita na kutokuwa na ukatili. lakini hata baada ya wanachama wa Umoja wa Mataifa kukubali kwa pamoja Siku ya Amani, mapambano bado yaendelea. Kwa kadri miaka inavyopita, hamna hata kusitishwa kwa vita kumoja. Sauti za wapinzani zinaendelea kupazwa na sasa shirika lisilokuwa la faida la Gilley, Peace One Day linahitaji msaada wa dharura wa kifedha. Lakini hawezi kuliacha shirika hili kushindikana. Himisho la kusisimua la filamu hii  linampata Gilley akiwa ameungana na Jude Law nchini Afghanistan wakijaribu kuasisi na kusimamia  chanjo kubwa dhidi ya ungonjwa wa kupooza  kwenye Siku ya Amani. Je, amani itadumishwa? Je, maisha yataokolewa? Au wale wapinzani walikuwa wakisema ukweli? Filamu hii ni angano linalosonga kuhusiana na nguvu za mtu binafsi na ustahimilivu wa moyo wa binadamu.

KUONYESHWA KULIKOPITA

Tunayo furaha sana kwamba Siku Baada ya Amani imepewa leseni ya kurushwa hewani kwenye nchi 96, pamoja na kuonyeshwa maalum zaidi katika pembe nyingi za ulimwengu.Tazama kuonyeshwa kulikopita hapa.

TAIFA LA FILAMU: SHORTS

Kwa ushirikiano na Panasonic, the Cultural Olympiad project Film Nation: Shorts ilizinduliwa mnamo Machi mwaka 2010 na ikaweza kuwaalika walio na umri kati ya miaka 14-25 kuweza kuunda filamu fupi ambazo zilisherehekea thamani ya michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu: heshima, ujasiri, ubora wa kipekee, urafiki, usawa, uamuzi na utiaji moyo. Mradi huu uliwapatia watengenezaji filamu fursa ya kuonyesha kazi zao katika michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu mnamo mwaka 2012 jijini London.

Mkurugezi wa Peace One Day Jeremy Gilley na Balozi Jude Law waliweza kuungana pamoja London 2012 katika kuzindua jambo jingine jipya katika mashindano hayo, pale ambapo vijana walihimizwa kuunda filamu fupi kutokana na kutiwa moyo kwa mada ‘Kusitisha vita’. Uwe ni utengenezaji filamu fupi kuhusu hali wanayopitia vijana katika kusitisha vita wakiwa na rafiki, au familia, au vile ambavyo usitishaji vita huu kama kitambo ama kwa sasa ulivyowatia moyo au kuleta utofauti katika maisha yao, ama kile ambacho usitishaji vita wa ulimwenguni kote ungemaanisha kwao kibinafsi, kwa ufupi London 2012 pamoja na Peace One Day ziliangalia filamu zilizo na hadithi za kutia moyo.

Taarifa zaidi kuhusu warsha zijazo na namna ambavyo unaweza kusajili yanapatikana katika www.filmnation.org.uk

 

Je, ulijua kwamba Peace One Day hutengeneza pia filamu kwa watu wengine? Pata kujua zaidi kuhusu kazi za filamu za Peace One Day hapa.

TUZO ZA SIKU BAADA YA AMANI

2008

Cannes

61st Festival of Cannes
-
Official Selection - Australia
Human Rights Arts and Film Festival
-
Official Selection - Sao Paolo
International Film Festival
-
Official Selection - Zagreb
Film Festival
-
WINNER
Cinèma Vérité Award

Paris and Geneva

WINNER
Best Documentary Award
Zimbabwe International Film Festival
-
Official Selection - Thessaloniki
International Film Festival
-
Official Selection - Stockholm
International Film Festival
-
Official Selection - Seville
Film Festival
-
Official Selection - Beirut
Né à Beryrouth
-
Official Selection - Kathmandu
International Mountain Film Festival
-
Official Selection - Nigeria
Abuja International Film Festival

Official Selection - Warsaw
Film Festival
-
Official Selection - South Africa
The Continents Film Festival
-
Official Selection
BritDoc Film Festival

2009

WINNER
Most Inspirational Movie of the Year
Cinema for Peace