Menu
Kwa nini utumie Peace One Day Productions
  • Huku tukiwa na uzoefu wa kufanya kazi ya kushinda tuzo kwa miaka 12 tumeweza kupata miunganisho ya kipekee katika kiwanda hiki.
  • Tuna uhusiano wa kuaminika na wandishi, watumiaji wa kamera na sauti, wahariri, vyumba vya habari na mafundi mitambo wa baada ya kazi ya mwanzo ulimwenguni kote.
  • Filamu zetu zimeweza kutangazwa ulimwenguni kote, sehemu hizo zikiwemo BBC2, BBC4 na BBC World.
  • Filamu zetu zote zinahaririwa ndani kwa ndani, hivyo basi zinawapatia wateja kiwango cha juu zaidi cha kufanyakazi nasi.
  • Mapato yote yanayopatikana kwenye Peace One Day Production yanawekezwa tena katika shirika lisilo la faida la Peace One Day. Wateja hivyo basi wanaunga mkono moja kwa moja suala hili la urasmishwaji wa Siku ya Amani ya Septemba 21.
Wateja Wetu

Tunafanyakazi na mseto wa wateja, kuanzia katika mashirika yaliyo na biashara katika nchi mbalimbali hadi katika miradi ya watu binafsi:

Skype

 

 Platinum Property Partners
 
Ushuhuda

"British Airways imefanyakazi na Peace One Day kwenye programu zetu nyingi za hivi karibunii. Katika wakati huu wote kundi letu limekuwa likiwapa msaada katika mtazamo wa ubunifu hadi uzalishaji kwa mujibu wa kuweza kuwashughulia rasilimali nyingi zinazomilikiwa na kampuni hii ya ndege kuanzia katika filamu ya hali halisi ya dakika 25 ikiangazia 4 mabingwa 4 wenye sifa kubwa zaidi katika kampuni hii ya ndege na hata nchi huku tukielewa  azimio lao katika michezo ya London ya 2012 kwa kuonyesha filamu fupi za kutangaza shughuli zilizokuwa zikifanyika pembeni na maono mbalimbali kuhusiana na kampeni yetu ya kutunzwa tuzo ya  "they will fly campaign.” Wao ni wepesi wa kujibu maswali yetu na wanajivunia sana kampuni yetu huku wakitaka kutayarisha kazi yenye ubora inayolingana na matarajio ya abiria na wateja wetu.” British Airways

 

 

"Mnamo mwaka 2009 kabla ya kufanyika kwa kwanza kwa  kombe la dunia la FIFA kwenye bara la Afrika, tukiwa na mshirika wetu FIFA, Coca-cola iliweza kusafiri kwenye bara lote ili kuweza kuwapelekea mashabiki wa kila nchi ya bara la Afrika Tuzo la Kombe la Dunia la FIFA kwa njia ya kipekee na ya kuvutia. Peace One Day Production iliweza kurekodi safari hii na kuchukua filamu ya kila hatua kwa ubora wa kipekee. Waliweza kutuma kazi iliyokamilika kwa muda na ndani ya bajeti iliyowekwa. Filamu hizi zilikuwa na athari kubwa na kiwango cha ubunifu kiligonga kikomo” Coca-Cola

Wasiliana nasi

Ili kupata kujua zaidi kuhusu kufanya kazi na Peace One Day Production tafadhali wasiliana na mojawapo ya  kundi letu:

Tutumie baruapepe katika: podproductions@peaceoneday.org

Tupigie simu kwa: +44 (0)208 334 9900