Menu

"Michezo inayo uwezo wa kubadilisha dunia ... ina uwezo wa kuhamasisha. Ina uwezo wa kuunganisha watu kwa njia ambayo kitu kingine hakiwezi. Inawaongelesha vijana katika lugha wanayoielewa. Michezo yaweza kujenga matumaini palipokuwa tu na kukata tamaa. Ina nguvu zaidi kuliko serikali katika kuvunja vizuizi kimbari."

Nelson Mandela

Kama unapenda michezo basi tumia nguvu zake kuvuka mipaka kwenye Siku ya Amani. Tunakukaribisha kuleta dunia pamoja katika maeneo ya michezo ya viwango vyovyote, kutoka ngazi za mashinani hadi kwa viwanja vikubwa, ili kuunganisha sio tu wachezaji na mashabiki,bali pia jamii na hata mataifa.

Ni rahisi, unalohitajika tu kufanya ni kuandaa tukio la michezo au kupitia kwenye bodi yetu tumia mojawapo ya mipango yetu ya michezo, na kumbuka kutujulisha ni mpango upi unaotaka kuutekeleza kwa kupitia barua pepe.

Michezo Shuleni

Elimu ya Peace One Day  inaleta amani darasani na rasilimali ya elimu ya bure .

Hii hapa ni mipango ya masomo mawili yanayowauliza vijana kutafiti nguvu za michezo nchini katika kuleta watu pamoja, ikiwa ni pamoja na mechi za soka zilizochezwa katika nchi isiyo ya mpinzini  wakati wa Krismasi katika Vita Vikuu vya  Kwanza vya Dunia na Kikombe cha Dunia cha Raga cha mwaka wa 1995 nchini Afrika Kusini.

Vidokezo vya Michezo ya Amani

Katika Mwaka wa 2015 ili kusherehekea na kuongeza uelewa wa Siku ya Amani  watu zaidi ya 49,000 walishiriki katika zaidi 5,000 ya shughuli za michezo  katika nchi 69 duniani kote, huku ikiwapa msukumo mamilioni zaidi.

Mexico

Kwa miaka kadhaa Tijuana Propone imekuwa ikiandaa matukio ya kufana sana ili kuongeza uelewa wa Siku ya Amani, na mwaka wa 2015 walipanga mashindano ya uendeshaji baiskeli  wa kilomita 6 na kushirikisha washindani 500 kutoka vilabu10  tofauti za uendeshaji baiskeli kwa kuongeza kwa mashindano ya kilomita10 ya magari 400 kutoka kwa vilabu 30 tofauti ya magari. Hatima ya shughuli zao ilikuwa kutembea kwa kilomita 3 usiku hadi mpaka wa Mexico hutu watu 8,000 wakiwa wameshika betri ya mishumaa na vijiti vya neon na kisha kuhitimisha katika hotuba kuhusu amani katika mstari wa kumalizia.

Liberia

Football to Develop Destitute (FODEDE) iliandaa uzinduzi wa mechi ya netiboli  mjini Monrovia ambapo wasichana wadogo walipata nafasi ya kujaribu bao la kwanza kabisa la netiboli nchini Liberia! Wasichana na wavulana walio na umri wa kutopita 17 & 12 pia walicheza mechi tatu za sokakwa ajili ya mpango wa Siku Moja Lengo Moja.

Iraq

Shirika lisilo la Kiserikali la Kurdistan Iraq NGO Network (IKNN) liliandaa mbio za kilomita 6 za Kimbia kwa sababu ya Amani huku watui  zaidi ya 1,000 wakishiriki katika mitaa ya Erbil na mashindano ya Soka ya One Day One Goal ya timu 10.

Kenya

Tangu mwaka wa 2008 Michezo ya Laikipia Highland yameadhimishwa kila mwaka kwa kutumia maadili ya kimsingi ya michezo katika kuendeleza mapenzi mema, kujenga mahusiano, kuzibamigawanyiko na kukuza vipaji vya wanariadha asili wa Kenya kushiriki katika mashindano ya amani juu ya Siku ya Amani, na mwaka wa 2015 haikuwa tofauti. Michezo hio hua ni mchanganyiko usio wa kawaida na wa kusisimua wa riadha na michezo ya kupendeza ya kitamaduni ya kabila mbali mabali yenye washiriki zaidi ya 3000 kutoka makabila 5 tofauti (Turkana, Kalenjin, Maasai, Kikuyu na Samburu)