Menu

Mambo Rahisi Yanaweza Kuimarisha Amani Mnamo Septemba 21 - Siku ya Amani

Maisha yetu yanajumuisha yale tunayopitia siku baada ya siku na hata yale tunayotangamana nayo, kwa hivyo kila siku tunayo fursa ya kuboresha maisha ya mtu mwengine. Ili kuimarisha ulimwengu wenye amani zaidi na ulio uendelevu, tunahitaji kuimarisha amani kwenye maisha yetu ya kila siku.

Haijalishi sisi ni wadogo kiasi gani, kila siku matendo ya upole yanaweza kusaidia kufanya amani kuwa uhalisi; ama kuwe ni kusimama kwa pamoja na mtu mwenye shida, kusema pole, kuungana tena na rafiki wa kitambo, au kusaidia mtu mwengine unayemwona kwamba ana haja ya kusaidiwa. Bila shaka matendo ya ghafla kama haya ya upole yanapaswa kufanyika mwaka mzima, hata hivyo tungependa kukualika kujiunga na wengine ulimwenguni kote kupatia wazo hili zuri lengo maalum kwenye Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21.

Popote pale ulipo, nyumbani, shuleni, au kazini, unaweza kusaidia kuboresha ubora wa maisha ya watu walio karibu nawe, wakiwemo familia yako, wenzako kazini, walimu, wale unaosoma nao au marafiki.

Wakati mwingine, mambo rahisi zaidi yanaweza kuwa na athari ya mara moja na yenye maana zaidi kwenye maisha ya kila mtu aliye karibu nawe.

Kwa hivyo kwenye Siku ya Amani ya mnamo tarehe Septemba 21…

Nini unaweza kusema ili kuridhia amani na mtu?

Nini unaweza kufanya ili kuridhia amani na mtu?

…nani utakayeridhia amani naye?

Maoni yako yatatusaidia kuweza kupima athari ya siku hii, na hivyo basi kuwapa moyo wengine kuweza kujihusisha.

Kwa hivyo tafadhali chukua muda kidogo kujaza Fomu hii ya Shughuli za 2014 hapa chini.