Menu
Kuhusu Peace One Day

Mnamo mwaka 1999, Jeremy aliasisi Peace One Day, shirika lisilokuwa la kupata faida, na mnamo mwaka 2001 jitihada za Peace One Day ziliweza kutuzwa wakati ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa kuwa pamoja waliipitisha siku hiyo ya mara moja kwa mwaka ya kusitisha vita ulimwenguni  kote na kutokuwa na vurugu mnamo Septemba 21-Siku ya Amani.

Lengo la Peace One Day ni kuweza kurasimisha  Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21, na kuifanya kuwa siku endelevu, Siku ya kila mwaka ya kuonyesha umoja ulimwenguni kote, siku ya ushirikiano wa baina ya tamaduni na kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana.

Jeremy Gilley ni mwigizaji aliyegeuka na kuwa mtengenezaji filamu, ambaye mwishoni mwa miaka  ya 1990 alijishughulisha na maswali kuhusu hali halisi ya umuhimu wa ubinadamu na swala la amani. Aliamua kuyachunguza maswali haya kupitia mbinu ya filamu, na hususan, kuunda filamu ya hali halisi kufuatia kampeni yake ya kuanzisha siku ya kila mwaka ya kusitisha vita na kutokuwa na vurugu.

Kwa kuunga mkono lengo hili, na akiwa alitiwa moyo na punguzo la asilimia 70 lilorekodiwa katika matukio ya vurugu ya mnamo mwaka wa 2007 nchini Afghanistan (chanzo: Idara ya Umoja wa Mataifa ya Usalama na Ulinzi), Jeremy alizindua misururu ya miseto ya Peace One Day, kila mmoja ukiwa na mshirika mwongozi:  Mseto wa mashirika yasioyokuwa ya kiserikari; Mseto wa Kupunguza ukali nyumbani ‘Mseto wa Wanafunzi ; Mseto wa Imani tofauti; Mseto wa Vyombo vya Habari; Mseto wa Kampuni; na ule Mtandao wa Shule.

 

Mwaka 2012 Peace One Day kumbukumbu ya athari za Siku ya Amani. Mchakato huu ulileta manufaa na ripoti ikaweza kutolewa ambayo iligundua, kote ulimwenguni, takribani watu milioni 280 katika nchi 198 walikuwa na ufahamu na Siku hii ya Amani ya mnamo mwaka wa 2012. Kwa Siku ya A mani mnamo mwaka wa 2013, kutokana na uzinduliwaji wa siku hii kwa kila sekta ya jumuia Ulimwenguni kote, Peace One Day ili rekodi ongezeko la 68% katika idadi ya wale walio kuwa na ufahamu na Siku hii yani watu milioni 470. Kati ya idadi hii, takribani asilimia 1-2% (milioni 4-8) walijiendeleza kwa Amani zaidi katika maisha yao ya kibinafsi kutokana na haya, na hivyo basi kuboresha ulimwengu kwa maelfu ya wengine.

Mnamo mwaka 2014 Ripoti ya Peace One Day iligundua kwamba zaidi ya watu bilioni 1 walifikiwa na ujumbe wa kuhusu Siku ya Amani. Kwa wale waliofikiwa, milioni 610 sasa wana ufahamu kuhusu siku hiyo, huku watu takribani milioni 10 wakiwa na mwenendo wa kuwa amani zaidi kutokana na hayo.

Maendeleo haya yameunda msingi thabiti wa kupeperusha ujumbe kuhusu Siku ya Amani kwa watu bilioni 3 kufikia mwaka 2016. 

Kupitia uanzilishi wetu binafsi na ushirikiano na wahusika mbalimbali, Peace One Day inaendelea kuhimiza mashirika na watu binafsi kuchukua hatua mahususi katika kupunguza vurugu katika mada: Nani Utariadhia Kufanya Naye Amani?

Mnamo mwaka 2014 Peace One Day imeweza kuzindua mradi wa miaka 3 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Eneo la Maziwa Makuu la Afrika kwa Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21. Lengo la mradi huu ni kuweza kuzidisha ufahamisho wa Siku ya Amani na kuzihimiza sekta zote kwa ujumla katika eneo hili kusimama pamoja  kwa ajili ya Amani mnamo tarehe Septemba 21. 

Peace One Day ni adilifu na ipo huru wala haitegemei serikali, ushawishi wa kisiasa, kampuni au imani yoyoye ya kidini. Kupitia katika mtazamo wa majukwaa mbali mbali, Peace One Day inatilia maanani nyenzo tofauti katika kuangazia ufahamisho, kutetea Siku ya Amani na kuhusisha jumuia ya kimataifa katika uadhimishaji wake mpana. 

 

Mwaka 2012 Peace One Day kumbukumbu ya athari za Siku ya Amani.

 

Wafadhili