Menu

Mpangilio wa Kupima

Mafanikio ya Peace One Day hayajaweka tu alama muhimu katika siku za usoni za Siku za Amani, bali yameweza kutilia mkazo thamani ya upekee wa siku hii ya kila mwaka na msingi wa amani endelevu ya muda mrefu. 

Jeremy aliweza kuzungumza na McKinsey & Company ili waweze kuunga mkono Peace One Day katika kuchanganua matokeo ya mnamo mwaka 2012. Mchakato huu ulisababisha uundaji wa mpangilio wa kupimwa ambao unawezesha Peace One Day kufuatilia ukuwaji wake katika shughuli za Siku ya Amani na athari inayohusika, hivyo basi kuisaidia kuendelea kuwasiliana na wote wanaohusika mwaka baada ya mwaka.

McKinsey & Company walitusaidia kuunda mpangilio wa ufanisi wa mabadiliko katika kampeni, na kulinganisha Siku ya Amani na jitihada nyingine za kijamii na za kikampuni ili kubadilisha tabia. Tunajua kwamba kwa kutekeleza mafunzo yaliotokana na kazi hii tunaweza kuendelea kuongeza idadi ya maisha yanayookolewa kwenye Siku ya Amani.

2015 - Matokeo

Ripoti ya Peace One Day ya mwaka wa 2015 inayoungwa mkono na McKinsey & Kampuni iligundua kuwa:

  • Inakadiriwa watu bilioni 1.5 waliweza kufikiwa na jumbe za Siku ya Amani kupitia shughuli kama densi na kampeni za vyombo vya habari
  • Duniani kote, watu milioni 709 walikuwa na ufahamu wa Siku ya Amani ya mwaka wa 2015
  • Kati ya wale waliokuwa na ufahamu, inakadiriwa watu milioni 13 walionyesha tabia ya amani zaidi siku hiyo - sawa na wakazi wote wa Chad
  • Takriban watu milioni 130 walifahamishwa kuhusu Siku ya Amani kupitia kampeni shirikishi za mitandao ya kijamii- mpango ya Umoja wa Mataifa wa #Samehekwasababu ya Amani na mpango wa Taasisi ya Amani ya Marekani ya #ChangamotoyaSikuyaAmani zilikuwa na hisia bilioni 2.
  • Shughuli za mashirika zilifahamisha watu karibu milioni 170 . Pendekezo la Amani la Burger King McWhopper kwa McDonald lilizalisha hisia zinazokaribia bilioni 9 na ndilo lililochangia zaidi kikuzalisha ufahamu wa Siku ya Amani ya mwaka 2015. Kampeni zingine kuu ni pamoja na vipengele vya kurasa wa Google, na wimbo wa kitaifa wa siku ya Amani wa Coca-Cola.

Peace One Day itaendelea kuhamasisha usaidizi na hatua katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, kwa kupitia msaada wa ukarimu wa Taasisi ya Howard G.Buffett.

Bonyeza hapo chini ili kusoma muhtasari wa ripoti:

 

Shughuli za Kuokoa Maisha za Siku ya Amani

Mikataba ya Siku ya Amani na wahusika wote kuhusiana na mgogoro nchini Afghanistan mnamo mwaka 2007 imesababisha kutolewa kwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza kwa watoto milioni 4.5 katika maeneo yaliodhaniwa kuwa hayawezi kufikika au ni magumu kufikika kutokana na mgogoro. Shughuli hii ya kampeni ya kutokomeza upoozaji imetokana na jitihada za pamoja za mamlaka ya afya ya Afghan, Shirika la Afya Dunia (WHO) na Mfuko wa Fedha wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) na ziliweza pia kusaidiwa na Kamati ya Kitaifa ya Msalaba Mwekundu pamoja na Mashirika ya Afya yasiyokuwa ya Kiserikali.

Kwenye Siku ya Amani ya mnamo mwaka 2008 katika nchi ya Afghanistan idara ya umoja wa mataifa ya Usalama na Ulinzi, ambayo inafuatilia matukio yanayohusiana na ulinzi, iliweza kurekodi punguzo la asilimia 70% katika matukio ya vurugu. 
Kwenye Siku ya Amani 2010, zaidi ya watoto 50,000 na wanawake wenye umri wa kupata watoto, kotekote katika maeneo 23 yenye hatari kuu ya sehemu kubwa ya Kabul, waliweza kupewa chanjo dhidi ya magonjwa hatari yakiwemo ugonjwa wa kupooza, uvimbe wa uti wa mgongo, dondakoo na pepopunda. Aidhaa, kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza ya kitaifa iliolenga watoto milioni 8 iliweza kuzinduliwa.
 
Shughuli za Siku ya Amani hazijawa tu kufanikiwa nchini Afghanistan. Mnamo mwaka 2010, Peace Day ilianzisha jumla ya shughuli za kibinadamu na za kuokoa maisha 88 kutokana na mashirika 28 Katika nchi 31. 
 

Shughuli za kibinadamu na za kuokoa maisha katika Siku ya Amani hufanyika duniani kote. Huwa zinachangia katika ujengaji amani, maendeleo na msaada, haya yote ni kama vile ugawaji wa nyenzo kama vile vyandarua vya mbu, chakula, na chanjo.