Menu
Sherehe za Peace One Day - Siku ya Amani 2014

Tafadhali angalia machapisho ya vyombo vya habari hapa chini ili kuona tangazo kuhusu Siku ya Amani  ya mnamo Septemba 21 mwaka 2014  yanayoendelea kule Goma, DRC.

“Uanzishwaji rasmi wa siku ya kusitisha vita ulimwenguni kote uliwakilisha kilele cha kazi ya miaka miwili ya mtengenezaji filamu wa Uingereza Jeremy Gilley, Aliyezindua mradi, unaoitwa Peace One Day, mnamo Septemba 1999.” - Kampeni
“Miaka Miwili baadaye Jeremy alikuwa ameungwa mkono kutoka kwa viongozi wa ulimwenguni katika kila bara na azimio la siku ya amani liliweza kupitishwa kwa wingi wa kura na Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 7 2001.” - The London Magazine
“Unapojenga nyumba, unaanza kwa tofali moja. Ukitaka kujenga Amani tunapaswa kuanza na siku moja. Siku yenyewe imefika.”  - Jeremy Gilley, Dallas Morning News