Menu
Kufanyakazi Kwa Pamoja Tunaweza Kuunda Peace One Day

Kuirasmisha Siku ya Amani na kuifanya kuwa yenye kujiendeleza yenyewe ndiyo maono ya kila mtu. Ili kuweza kuongeza zaidi kushiriki kwa watu ulimwenguni kote na kuwezesha makundi mingine ya wahusika wengine kuimiliki siku hii, Peace One Day imeunda misururu ya miseto ya ulimwenguni kote. Miseto hii inajumuisha mashirika husika ambayo yamejitolea katika kufanya shughuli kwenye Siku hii ya Amani na kuhusisha mitandao yao ulimwenguni kote. Mashirika ya ndani ya kila sekta yanao uwezo wa kuunganisha ujumbe na shughuli zao kwa kuunga mkono Siku ya Amani, na hivyo kufikia athari kubwa zaidi. Aidha Mtandao wa Shule ni fursa ya taasisi za kielimu na walimu kuweza kuja pamoja kwa kuunga mkono Siku ya Amani. Wanachama wa miseto hii na Mtandao wa Shule vyote vinakua kwa haraka.

Kupitia katika uanzilishi na ushirikiano na wahusika mbalimbali, Peace One Day imedhamiria kuhimiza mashirika na watu binafsi kuchukua hatua maalum za kupunguza vurugu ulimwenguni kote kwenye mada: Nini utakayeridhia amani naye?

 

Tujulishe Mipango Yako ya Siku ya Amani!

Kujiunga na mojawapo ya miseto ya Peace One Day ni njia madhubuti ya kukuza ufahamisho na kuungana pamoja katika Siku ya Amani. Hata hivyo usisahau kutuambia mipango yako ya siku hii. Ukifanya hivi unatusaidia kupima athari ya siku hii, na kuwapatia moyo wengine kushiriki. Tafadhali chukua dakika chache kukamilisha Fomu ya Shughuli za 2014 hapa chini. 

Mseto wa Kampuni

Ili Peace One Day iweze kuendeleza na kuongeza ukuzi wa shughuli za Siku ya Amani kote ulimwenguni kiwango kipya kinahitajika kutoka kwenye sekta ya kampuni. Mashirika yanaweza kufungua uwezo wao wa watumiaji na kuwa na nguvu za uhamasishaji, pamoja na kuvuta pamoja wahusika wake wakuu pamoja na waundaji maoni na viongozi wa biashara, n.k. Hii ni fursa ya kuchangia katika jumuia kwa njia nzuri. Uandikishwaji wa uanachama wa kila mwaka usiobadilika, lakini wa bei nafuu na kujitolea katika kuhamasisha msingi wao wa watumiaji pamoja na wafanyakazi kutawezesha mashirika kufaidika na uhusiano wao na Peace One Day katika idadi kadhaa za majukwaa na kuwa sehemu ya kundi ambalo bila shaka litarasmisha Siku ya Amani ulimwenguni kote.

Mseto wa Wanafunzi

Mseto wa Wanafunzi wa Peace One Day unawaleta pamoja wanafunzi kutoka duniani kote kuweza kuadhimisha Siku ya Amani ya Septemba 21. Kampeni hii ni fursa ya kipekee ya jumuia ya wanafunzi wa kimataifa kuungana pamoja na kuchukua hatua kuliko vile ambavyo wamewahi kuchukua. Tafadhali tumia mtandao wa kijamii na mitandao mingine kutusaidia kueneza ujumbe na kujenga msukumo wa kampeni hii iliyo mbele yetu ya Siku ya Amani. Bofya filamu hii iliyo mkabala ili kuona uzinduzi wa mseto huu wa mnamo mwaka 2012 utakaokupatia moyo.

Mseto wa ‘Kupunguza Ukatili wa Nyumbani’

Siku ya Amani ni fursa ya kuungana kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana na kuweza kupatia suala la ukatili wa nyumbani kipaumbele. Wakfu wa Kimataifa wa EDV ndio mshiriki mkuu katika mseto wa ‘kupunguza ukatili wa nyumbani’ ambao unaleta pamoja mashirika ya watu binafsi kutoka pembe zote za ulimwenguni, ambao wamejitolea katika kupunguza ukatili wa nyumbani kwenye Siku ya Amani. Bofya filamu iliyomkabala hapa ili kuona uzinduzi wa mseto huu wa mnamo mwaka 2012 utakaokupatia moyo.

Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali

Siku ya Amani ni fursa ya kila mwaka kwa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali kuweza kuangazia kwa umakini zaidi shughuli zao zinazoendelea za uimarishaji wa amani na za kuokoa maisha ndani ya muktadha wa ulimwenguni mzima. Interpeace, Mojawapo la Shirika Lisilokuwa la Kiserikali kubwa zaidi ulimwenguni linalolenga katika kuimarisha amani, ndilo mshiriki mkuu katika mseto huu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, ambao unaleta pamoja Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali kutoka kote ulimwenguni katika kuunga mkono Siku ya Amani. Bofya filamu iliyomkabala hapa ili kujua zaidi kuhusu mseto huu.

Mseto wa Kidini

Watu wengi zaidi duniani wanajitambulisha kuwa sehemu ya imani, mazoea ya kiroho au kundi la kidini. Kwa kuitikia huku kwa kipekee kwa makundi ya kidini katika shughuli ya Siku ya Amani ya mnamo mwaka 2012, Peace One Day inazindua mseto wa kidini, unaoyawezesha Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali lakini ya kidini, makundi ya imani tofauti tofauti, makundi wakilishi, vijana na viongozi wa kidini mashinani, sehemu za kuabudu, na watendakazi wa kidini na kiroho wa imani zote, mifumo ya kuamini na madhehebu ulimwenguni kote kuweza kuungana pamoja katika Siku hiyo ya Amani ya Septemba 21.