Menu

Kukiwa na maoni mingi sana kuhusu wajibu wa dini ambayo yanagongana, wajibu wa kiroho katika kuimarisha amani mara nyingi huwa unapuuzwa.  

Tafadhali jiunge na Dini kwa ajili ya Amani Kimataifa (Religions for Peace International - RfP), Kamati ya Elijah ya Vingozi wa Kidini Ulimwenguni (Elijah Board of World Religious Leaders), Baraza la Ulimwengu la Viongozi wa Kidini (World Council of Religious Leaders) na mashirika mingine mingi katika kuwaalika waumini wa kidini wa ulimwengu katika kuadhimisha hali ya kiroho ya masaa 24 kwa ajili ya amani, kutokuwa na vurugu na kusitisha vita katika Siku ya Amani, ya mnamo Septemba 21.

Athari ya siku hii ya kusitisha vita na kutokuwa na-vurugu kote ulimwenguni inaweza kuwa kubwa. Shughuli ya Siku ya Amani nchini Afghanistan tangu mnamo mwaka 2007 imeweza kusababisha kufanyiwa chanjo dhidi ya ungonjwa wa kupooza watoto milioni 4.5 katika maeneo ambayo awali yalidhaniwa hayawezi kufikika au yalikuwa magumu kufikika kutokana na mgogoro na hivyo basi kuonyesha kwamba hatua shirikishi kwenye siku hiyo huokoa maisha.

Kama ungependa kuungana na watu wengine wenye akili sawa na zako na mashirika yanayoshiriki katika  Siku ya Amani katika eneo lako, au una maswali, tafadhali wasiliana na mwanachama wa kundi la Peace One Day katika faith@peaceoneday.org.

Amani Inawezekana tu Kutokana na Ushirikiano wa Imani Tofauti Ulimwenguni

Wafuasi wa imani tofauti wanaweza kuishi kwa pamoja na kuheshimiana na kuelewana. Wana mingi ya kusaidiana, wakichukua kutokana na urithi wao wa kiroho, ili kusaidia kuunda jumuia iliyokita mizizi katika maadili ambayo yanaendelezwa kwa pamoja kati ya imani teule za kihistoria.

Jumuia za kidini ndizo kubwa zaidi na zilizojipangilia zaidi katika taasisi za kiraia ulimwenguni, zinazodai kuwa na wafuasi wafikao mabilioni katika jamii tofauti, madaraja na hata migawanyiko ya kimataifa. Ulimwengu wenye amani unawezekana tu pale ambapo waumini  wa ulimwengu huu wa kidini na kiroho watakuja pamoja na kushirikiana.

Jiunge na Vuguviugu

Jiunge na vuguvugu linaloitisha hali ya kusitisha vita na kutokuwa na ukatili ulimwenguni kote katika Siku ya Amani.

Ninajitolea katika kuadhimisha kiroho suala la amani, kutokuwa na vurugu na kusitisha vita katika Siku ya Amani, ya mnamo Septemba 21.

Nani Utakayeridhia Amani Naye?

Mnamo  Septemba 21 mwaka 2013 Katibu Mkuu wa Kimataifa wa Dini kwa ajili ya Amani (Religions for Peace International) alikuwa mwenye kiti wa jopo la washawishi wachanga wa kipekee na wenye nguvu sita na ambao walitoka katika tamaduni za kidini sita tofauti na kwenye sekta ya jumuia. Washiriki walitafakari kuhusu wajibu wa kiroho katika maridhiano na ujenzi wa jamii, na kuchunguza ambavyo siku ya kila mwaka ya amani inaweza kutumiwa na kizazi kipya cha waumini wa kidini ili kuweza kujenga mapatano.

Mwenye kiti alikuwa: Dr. William F. Vendley – Katibu Mkuu wa Kimataifa wa Dini kwa ajili ya Amani

Washiriki: Frank Fredericks – Mwasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Imani ya Ulimwenguni kote na Mwasisi mwenza wa Uhuru wa Kidini Marekani; Khalid Latif – Mkurugenzi Mkuu wa  kituo cha Kislamu katika Chuo Kikuu cha New York na Kasisi wa Idara ya Polisi ya Jiji la New York City;  Samantha Bloom - Kamati ya Uongozi wa Vijana, Kamati ya Wakurugenzi kwa ajili ya Mbegu za Amani na  Ofisi ya Kampuni ya Kuhusisha kwa ajili ya benki ya mataifa mbalimbali;  Kinjal Dave – Kizazi Kinachofuata kiongozi wa Seva  kwa ajili ya Wahindi  Marekani jumuia za Seva na kiongozi mkuu wa vijana wa imani tofauti; Doyeon Park – Mwakilishi Badali wa Won Buddhism katika Umoja wa Mataifa na mweka Hazina wa Kamati ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali ya Kidini katika Umoja wa Mataifa; Simran Jeet Singh – Msimamizi Mkuu wa Kidini wa Mseto wa Sikh na Mwenyekiti wa Kamati ya Imani Tofauti za Baraza la Ulimwenguni la Sikh.