Menu
Filamu za Peace One Day

 

Ukatili Mkubwa Zaidi Ambao Binadamu Wanakumbana Nao ni Ukatili wa Nyumbani

Siku ya Amani inahusu vilevile pia ukatili katika nyumba zetu, jamii na shule zote kwani ni juu ya vita vya kiraia na kimataifa. Kama watu binafsi watakuja pamoja kwenye siku hii, ukatili zaidi utaweza kuzuiliwa kuliko kama vita vyote vitasitishwa kwa wakati mmoja.

Wakiwa na mshiriki mwongozi, Wakfu wa Kukomesha Ukatili wa nyumbani na Ulimwenguni kote na mwasisi wake Baroness Scotland QC, Peace One Day imeweza kuwaweka pamoja washiriki wa mseto huu ambao waliojitolea katika kupunguza ukatili wa nyunbani ulimwenguni kote katika Siku ya Amani.

Kulingana na kampeni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ungana Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake, kwa wastani, angalau mwanamke mmoja kati ya watatu anapigwa, analazimishwa kufanya mapenzi au vinginevyo ananyanyaswa na mwenzi wa karibu kimwili katika mkondo wa maisha yake. Miongoni mwa wanawake walio na umri kati ya 15 na 44, vitendo vya ukatili husababisha hali nyingi zaidi za vifo na ulemavu kuliko hata saratani , malaria, ajali za foleni na vita vyote vikiwekwa pamoja (Benki ya Dunia). Nusu ya wanawake wote wanaokufa kutokana na mauaji ya kikatili nyumbani wanauawa na mwenzi wao wa sasa au wa awali (WHO/ Benki ya Dunia). ‘Ukatili wa Nyumbani hufanyika ulimwenguni kote, na hivyo basi huathiri mamilion ya watu katika jamii nzima, haijalishi ni kiwango kipi cha uchumi kwao. Hakuna nchi au jumuia ambayo haijaguswa’ Baroness Scotland QC. Kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu unayemjua ameathirika na ukatili wa nyumbani katika maisha yake.

Ukatili wa nyumbani huathiri familia na jumuia zote. Katika Uingereza pekee, kati ya watoto 750,000 na 950,000 wanatoa ushahidi kuhusu ukatili wa nyumbani kila mwaka, na ambao huathiri maendeleo yao kielimu na afya (UNICEF na ripoti ya Bodyshop International).

Siku ya Amani itakuwa ni fursa ya kuungana katika kiwango ambacho hakijawahi onekana awali na kuyapa kipaumbele masuala ya Ukatili wa nyumbani. Pamoja tunaweza kupunguza kiwango cha ukatili, kukuza ufahamisho na kuzalishwa shughuli kadhaa na mseto karibu na masuala hayo.

Nani Utakayeridhia Naye Amani?

Siku ya Amani ya tarehe 21 Septemba 2014

Mnamo mwaka 2013, Peace One Day iliweza kuzindua mada ya Siku ya Amani, mnamo Septemba 21: Nani Utakayeridhia Naye Amani?

Amani huanza na hatua ya mtu binafsi, na hatua zako huwapa moyo wengine kufanya vivyohivyo. Siku ya Amani ya tarehe Septemba 21 ni fursa kwetu sote kuanza kujihusisha katika mchakato wa amani na familia, rafiki na jumuia zetu.

Kwa kufanya kazi pamoja na kuridhiana amani baina yetu tunaweza kuboresha ubora wa maisha yetu. Siku ya Amani si tu kuhusu kupunguza ukatili katika maeneo ya mgogoro, bali ni kuhusu kupunguza ukatili katika nyumba zetu, jumuia na shule zetu.

Kwa hivyo ni nani utakayeridhia naye amani? Nani utakayekuja naye pamoja kwenye Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21 mwaka 2014?

Yafuatayo ni yale unayoweza kufanya:

1. Bofya hapo juu ili kujiunga katika mseto sasa  
2. Kuza ufahamishio wa Siku ya Amani
3. Chukua hatua mnamo Jumamosi Septemba 21, mwaka 2014

Kwa mawazo na rasilimali za kusaidia kukuza ufahamisho wa Siku ya Amani na kuanza kujihusisha katika kampeni tembelea ukurasa wa Rasilimali.

Uzinduzi wa Hafla – Machi 21, 2012

Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21 ni fursa ya kuunganisha kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tena awali na kuleta mbele suala ya Ukatili wa Nyumbani. Jiunge na ‘mseto wa kupunguza ukatili’, wakati una adhimisha Siku ya Amani ya mwaka 2014 kwa njia fulani na tufahamishe kuhusu hilo.

Uzinduzi wa Hafla – Machi 21, 2012

Peace One Day na wakfu wa kukomesha Ukatili wa Nyumbani wa Kimataifa (EDV) wote waliheshimika kwa kukaribisha jopo la wakilishi kutoka kwa mashirika yanayoshughulikia Ukatili wa Nyumbani kutoka ulimwenguni kote katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mseto wa‘Kupunguza Ukatili wa Nyumbani’ mnamo Machi 21, 2012 jijini London, Uingereza.

Tuna furaha kujua kwamba Balozi wa Peace One Day Jude Law na Thandie Newton walijiunga nasi katika hafla hii.