Menu
Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Unaunganisha Kwa Kutumia Amani

Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali unayaleta pamoja Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali yenye maono sawa ambayo yangependa kuangazia haja ya amani na kile ambacho kinaweza kufikiwa kwa kutumia amani. Hii inamaanisha kwamba Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ya amani, ubinadamu na maendeleo yanazidi kuongeza majina yao katika Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali, na kuonyesha msaada wao kwa ajili ya amani na kwa ajili ya kampeni ya Peace One Day Nini utakayeridhia amani naye?

Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali unaongozwa na Peace One Day pamoja na NGO Interpeace ya Kimataifa. 

“Kile nilichopenda zaidi kuhusu wazo lake Jeremy la sisi kuunga mkono Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali kilikuwa kwamba hatutakuwa tukizungumza tu na Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali yanayolenga kudumisha amani bali Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ambayo yanahitaji amani hili kuweza kufanya kazi zao za kibinafsi za ubinadamu, misaada au maendeleo.” 

Scott M. Weber, Mkurugenzi Mkuu, Interpeace.

Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali huyaleta pamoja mashirika kutoka ulimwenguni kote ambayo yamejitolea katika kuadhimisha amani mnamo Septemba 21 katika Siku ya Amani kupitia katika kazi zao. Wanachama wa mseto wanaweza kufikiana kila mmoja wao na kuungana kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana. Kwa pamoja tunaweza kupunguza kiwango cha ukatili, kukuza ufahamu wa shughuli zetu na kuokoa maisha ulimwenguni kote.

Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali unaendelea kukua na hivi sasa kuna Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ya kitaifa na mataifa ambayo yameandikishwa kutoka kila bara. Orodha kamilifu ya wanachama inaweza kupatikana hapa chini. Kwa sasa Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali umefikia jumla ya wanachama 835 kutoka katika nchi zaidi ya 140.

Ukiwa umetiwa moyo na punguzo lililorekodiwa la asilimia 70% katika matukio ya ukatili katika Siku ya Amani nchini Afghanistan (chanzo: Idara ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi na Usalama), Mseto wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ulizinduliwa mnamo mwaka 2012. Wanachama waasisi ni pamoja na Interpeace, BRAC UK, MAG (Kundi Shauri la Migodi), Mercy Corps na War Child. ACCORD na Viva Rio. Martin Bell, aliyekuwa mwanahabari wa vita wa kushughulikia masuala ya vita BBC na Balozi wa utu wema wa UNICEF na Emmanuel Jal, aliyekuwa askari mtoto pamoja na mwana muziki wa Sudan Kusini, waliongea katika uzinduzi wa hafla hii London.

Tangu hapo, mamilioni ya watu wamekuwa wakishughulikia Siku ya Amani katika kila nchi ya ulimwengu, na mamia ya mashirika yameweza kutekeleza na kuokoa maisha katika maeneo ya mgogoro. Hapo chini unaweza kusoma zaidi kuhusu athari ya kazi yetu nchini Afghanistan.