Menu

Unga Mkono Peace One Day na Eneza Ujumbe wa Siku ya Amani ya Mnamo Septemba 21

Tunakuomba kuanza kujenga mseto wako binafsi wa mashabiki na kupangilia namna ambavyo mtakavyokuja pamoja mnamo Septemba 21 mwaka 2014, katika chuo kikuu chako, katika mji wa nyumbani kwenu au popote pale utakapokuwa. Umoja wa Mataifa unahusika katika mchakato huu. Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali yanahusika katika mchakato huu. Lakini ni kujitolea kwa wanafunzi na vijana katika kuja pamoja kwa idadi kubwa katika Siku ya Amani ya mwaka 2014 ambako kutaleta ile nguvu na mshikamano unaohitajika katika kutia moyo serikali ili ziweze kufuata.

Unaweza kukuza ufahamisho huu kabla ya Siku ya Amani kwa kupangilia shughuli katika chuo kikuu, shule au jumuia yako ambazo zitawahimiza wengine kutiwa moyo na kujiunga na kampeni ya Peace One Day ili kurasmisha Siku ya Amani. Baadhi ya shughuli za kukuza ufahamisho zinajumuisha uonyeshaji filamu, makongamano na shughuli za darasani. Kwa mawazo zaidi tembelea ukurasa wetu wa jumuia.

Kwa hivyo nani utakayeridhia naye amani? Nani utawaleta pamoja katika Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21 mwaka 2014?

Yafuatayo ni yale unayoweza kufanya:

1. Bofya hapo juu ili kujiunga na Mseto wa Wanafunzi sasa 
2. Kuza ufahamisho wa Siku hii ya Amani  
3. Chukua hatua mnamo Jumapili Septemba 21, mwaka 2014

Kwa mawazo na rasilimali za kusaidia wa kukuza ufahamisho wa Siku hii ya Amani na kuhusika katika kampeni tembelea ukurasa wa Kuchukua Hatua