Menu
Filamu za Peace One Day

Ifuatayo ni misururu ya filamu ambazo zinaainisha elimu ya Peace One Day

Rasilimali Maalum Mtalaa

Moja kwa moja katika darasa lako: Zungumza naye Jeremy Gilley, mwasisi wa Peace One Day, au mojawapo wa mabalozi katika darasa lako kupitia Skype. Peace One Day inatumia Skype ili kuunga watu madarasani kote ulimwenguni. Hii inajumuisha miradi ya mazungumzo ya Skype na mazungumuzo ya Amani. Kwa taarifa Zaidi na kujiandikisha katika mazungumzo ya Skype, tafadhali bofya katika kitufe kilicho hapa chini.

Skype Projects 

Jiunge na Mtandao wa Shule na utusaidie kuhamasisha kizazi cha vijana wanaounga mkono Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21!

Jina la Shule yako litaonyeshwa katika orodha hii ya mtandaoni.

Your school's name will be displayed on an online list.
Mtandao wa shule

Umri wa miaka 11-18 
Sekondari ya Uingereza

UK
View Full Version
Download Full Version
Download Print Version

Umri wa miaka 5-11 
Msingi ya Uingereza

UK
View Full Version
Download Full Version
Download Print Version

 
Umri wa miaka 11-18 
MAREKANI

USA
View Full Version
Download Full Version
Download Print Version

Umri wa miaka 11-18 
KOLOMBIA

COLOMBIA
View Full Version
Download Full Version
Download Print Version

Hususan kwa Waelimishaji /Walimu

Moja kwa moja kwa darasa lako: Zungumza na Jeremy Gilley, mwasisi wa Peace One Day au mmojawapo wa balozi katika darasi lako kupitia Skype. Peace One Day hutumia skype ili kuunganika na watu madarasani kote ulimwenguni. Hii inajumuisha miradi ya mazungumzo ya Skype na mazungumzo ya Amani. Kwa taarifa zaidi au kujiandikisha katika mazungumzo ya skype, tafadhali bofya kitufe kilicho hapa chini.

Mabalozi wa Elimu

Kufuatia ufanisi wa Siku ya Amani ya mnamo mwaka wa 2012, tungependa kupanua elimu ya Peace One Day na kuweza kufikia matokeo makubwa zaidi katika mwaka 2014. Ule utafiti wa Siku ya Amani 2012, uliweza kufanywa kutokana na msaada wa McKinsey & Company, na ukaonyesha namna ambavyo vijana wanaongoza katika mchakato wa kuifanya rasmi Siku ya Amani mnamo Septemba 21. Tulizindua Programu ya Balozi wa Elimu ya Peace One Day ili kuendeleza ufanisi huu.

Programu hii inaunganisha vielelezo vyenye kutia moyo kutoka katika mseto wa nyanja mbalimbali zikiwemo filamu, muziki, ufundishaji na hata sekta ya kampuni zikiwa na vijana kutoka duniani kote.  Mabalozi hawa watatumia skype ili kugawiza hadithi zao za Peace One Day katika shule na makundi ya vijana. Programu hii itawatia moyo vijana kujihusishwa katika mchakato wa amani na kuwa kizazi kijacho cha waendelezaji amani.

Kwa kupata kujua zaidi kuhusu kila Balozi tafadhali bofya katika picha zilizo hapa chini

Mtandao wa Shule

Jiunge na mtandao wa shule na mtusaidie kuhamasisha kizazi cha vijana katika kuunga mkono Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21! 

Jina la shule yako litaonyeshwa kwenye orodha ya mtandaoni.

Friend Our World (Rafiki wa Dunia yetu)

Ilizinduliwa mnamo mwaka wa 2013, Septemba  Rafiki wa Dunia Yetu, ni kitovu cha kujifunza mtandaoni kwa watoto kinacho unganisha michezo ya urafiki ya jiogarafia, lugha na uraia wa kote ulimwenguni. Kuwa sehemu ya  milioni  ya watoto watakao kuja pamoja katika hali halisi ya  "Wacha tuwe marafiki."

Rafiki wa Dunia Yetu inaundwa na Skoolbo kwa ushirikiano na Peace One Day na Microsoft.

 

skype in the classroom logo

 

 

Kama wewe ni mwalimu na ungependa kuunganisha wanafunzi wako katika madarasa mingine duniani kote kwa mabadilishano ya kirafiki tembelea skype katika darasa na ujisajili ili kushiriki katika kipindi cha Rafiki wa Dunia Yetu. 

Ushuhuda

"Uraia wa Kujishughulisha ni mada kuu katika mtalaa wa uraia. Peace One Day ni shirika, azimio la Umoja wa Mataifa, furushi la lasirimali na siku ya Amani yenyewe vyote ni matokeo ya wazo ya mtummoja na bidii ya kulifanya wazohilo kuwa la uhalisia. Furushi la rasilimali ya Peace One Day linatilia maanani suala hili na kulitumia, na mifano mingine, ili kuruhusu wanafunzi kugundua fursa za watu binafsi na kuzileta na hivyo basi kuleta mabadiliko ya kijamii. Dhana hii inaingiliana moja kwa moja na kushiriki pamoja na uwajibikaji wa  sehemu ya kuchukua hatua katika mtalaa wa uraia na inaweza pia kutumiwa katika kutilia mkazo umuhimu wa kupiga kura na kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia. Kuna mipango ya vipindi vingi ambayo inaunganishwa na sehemu nyingine za Programu ya Uraia wa masomo ya Hatua kuu 3 na 4 zikiwemo kuwafundisha wanafunzi kufikiria kuhusu masuala yenye mada, ya kisiasa, kiroho na maadili pamoja na ya kijamii na hata kitamaduni, matatizo na matukio husika. Wanafunzi wanahimizwa pia kuchangia katika mazungumzo ya makundi na ya uchunguzi, na kushiriki pia katika mijadala. Baadhi ya mipango ya vipindi inaangalia kazi za umoja wa mataifa, ambazo zinaweza kutumiwa kama kianziyo cha kuchunguza taasisi zingine za kidemokrasia. Pia kuna taarifa na mawazo chungu nzima ya kushugulikia yanayogusia masuala ya dhuluma, kujifunza, kusuluhisha mgogoro bila upendeleo, haki za kibinadamu na kihalifu."
Elaine Sweeney, Serekali ya Uingereza, Idara ya Elimu & Mbinu, PSHE & Kundi la Uraia, Uingereza

"CISV Kimataifa ni shirika la Elimu la Amani la kote ulimwenguni, linalofanya kazi katika zaidi ya nchi 60 kote ulimwenguni. Tumefurahishwa sana na Rasilimali ya Kimataifa ya Peace One Day ambayo itakuwa ikitumia mipango ya vipindi na rasilimali nyingine kuhusu Mgogoro na Usuluhishaji katika Programu zetu zote za Elimu ya Amani kwenye mwaka ujao. Wenzetu waliojitolea mhanga duniani kote wana furaha isiyo na kifani kuhusu matumizi ya rasilimali hii ya Kote Ulimwenguni, kwani ni ya ubora ya kiwango cha juu na inaweza kutiliwa maanani kwa urahisi katika matumizi ya hali isiyokuwa rasmi, na isiyokuwa ndani ya darasa kwa watoto na vijana kutoka katika mazingira tofauti ya kitaifa na kitamaduni. Tumefurahi kwamba pia Rasilimali ya Kimataifa inapatikana pia katika lugha tofauti na hivyo husaidia kuhakikisha kwamba  inaweza kufikiwa na wote."
Kiran Hingorani, Afisa wa Elimu,  CISV International

"Asante sana kwa kuhakikisha kwamba nyenzi hii ya rasilimali muhimu sana inapatikana kwetu. Masuala yaliyomo katika vipindi hivi (Amani, kutokuwa na vurugu, usuluhishaji wa mgogoro, uraia wa kote ulimwenguni, ushirikiano wa kati ya tamaduni n.k.) ni muhimu sana kwetu sisi Wasomali."
Ahmed Ibrahim Awale, Mtandao wa Uimarishwaji wa Elimu Somali 

"Rasilimali ya elimu ilikuwa yenye msaada sana na ya kusisimua akili na tuliitumia kama msingi wa kazi ya warsha ya siku mbili thabiti kwa wanafunzi wetu wa sekondari, pamoja na njia ya kuwapatia moyo katika shughuli ambazo wanafunzi wetu wa shule ya msingi walihusika. Ilithibitishwa kuwa kichochezi mwafaka cha kuangazia ufahamisho kamili.”
Mark Angus, Kinara, Shule ya Kimataifa Uingereza,  Nanxiang, Shanghai

"Hapa katika shule yetu ya wilaya tunalenga katika kuunda fursa zinazofaa na kamilifu kwa wanafunzi wetu. Shughuli mara nyingi zinafuata msingi wa mradi na zinayo matarajio ya kijamii, kiakademia na kiteknologia. Wanafunzi katika darasa la 8 na 12 wanahitajika kukamilisha mradi wa kujifunza katika kutoa huduma kwenye jumuia. Mtalaa huu unasaidia sana katika kutekeleza aina hii ya kazi na uunganishi katika nyanja nyingi za mtalaa wetu katika masomo ya kijamii (historia, jiografia, uchumi, dini, tamaduni, wajibu wa kiraia n.k.) na kujua kusoma na kuandika” 
Aron Merrill, Mwalimu, Shule ya Kati ya Williston, Burlington, VT, Marekani

"Katika Shule ya Upili ya Port Glasgow tuliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Amani mnamo Septemba 21. Mojawapo ya matokeo makubwa zaidi ya siku hii yalikuwa ni namna ambavyo tabia ilivyobadilika pakubwa katika siku hiyo, kutokana na kupendekezeana, katika hali ya wafanyakazi na wanafunzi kuwa wema kati yao.”     
Lorna Anderson, Mwalimu, Shule ya Upili ya Port Glasgow , Scotland, Uingereza

"Kutazama DVD kulibadilisha, kukapanua na kuimarisha mitazamo yangu kuhusu Amani. Nikiwaona wanafunzi wangu wakionyesha hisia kama walivyopaswa, ilikuwa ni uzoefu mzuri sana kwangu. Hawa ni watoto wakakamavu, wanafunzi ambao wana mambo machache sana ya kusaidia ukuaji wao. Hawaishi katika  ulimwengu wenye amani. Lakini nyenzo hizi ziliwagusa zikawapa ujasiri wa kuongea maoni yao na zimebadilisha tabia yao kuwa bora zaidi… na kwa kusema ukweli nilipata nyenzo hizi kuwa bora zaidi ambazo sijawahi kukutana kwa miaka ambayo nimekuwa mwalimu.”  
Debora Ghoreyeb, Mwalimu, Shule ya Upili ya Capital, Santa Fe, NM, Marekani

"Peace One Day…huwawezesha watoto wa karne ya 21 kuweza kuchambua masuala maalum ya amani na vita na yale ya amani na haki katika mdahalo wazi, bila ya masomo yao kubakia tu katika nadharia ya kuunga au kupinga vita.”   
Terence Copley, Mwalimu wa TES, Uingereza

"Walimu hapa wamekuwa  wakiuliza maswali mengi baada ya kitu hiki (Rasilimali ya Marekani). Furaha yao isiyo na kifani inasisimua sana, na inafanya kueneza ujumbe huu kuwa wenye furaha pia. Nitahakikisha kwamba habari hizi zinawafikia wanafunzi wa shahada ya kwanza na wahitimu, vilevile. Nadhani kwamba habari hizi zitaenea kama moto wa kichakani, kwa kusema ukweli.”
Stefanie Kendall, Mwanafunzi wa Uzamifu, Chuo Kikuu  cha  Jimbo la Michigan, MI, Marekani

"Mwanafunzi mmoja shuleni (Na utilie maanani kwamba watoto hawa wanatoka kwenye shule yenye Ugumu wa Kihisia na Kitabia, wote walio na mwegemeo wa vurugu) aliniambia kwamba badala ya kumkasilikia baba yake, jambo ambalo kwa kawaida yeye hufanya, yeye hujitenga na kutafakari yale yanayo mkasilisha! Mafanikio kama haya yanafikiwa tu kupitia katika uanzilishi unaotokana na kazi ngumu kama hii yenu. Kwa kweli inafanya kazi.”
James Cootes, Mwalimu, Shule ya Mount Tamar, Uingereza

"Asante Jeremy kwa kutukumbuka sisi miongoni mwa wengi hapa New Hampshire. Wanafunzi wangali wanazungumzia kuhusu Peace One Day. Paul na mimi tayari tumejisajili katika tovuti ya elimu na huwa tuna pakua rasilimali. Na zinapendeza. Tunaanzisha kitengo cha ushauri mwaka ujao na tunapangilia kutumia baadhi ya vipindi kwenye ushauri huo kwanzia siku ya kwanza ya shule ili kuwafanya wanafunzi kuchangamkia mnamo Septemba 21. Tunagawiza tovuti hii kwa wafanyakazi wote pamoja na wale tunaowajua nje ya shule.”
Tricia Taylor, mwalimu wa Shule ya Upili ua  Stevens, Claremont, NH, Marekani

"Unaona vita, uhalifu wa wahuni na mauaji kwenye televiseni kila wakati. Nafikiri kwamba Siku ya Amani itamanisha uonevu kidogo na pia itaweza kupunguza uhalifu kwa sababu siku hiyo itaangazia ufahamisho huu wa amani. Sasa nikiona mtu yeyote akidhulumiwa ningependa niende hapo na nisitishe tukio hilo.    
Ayman Khokhar, umri wa miaka 13, Uingereza

"Tumaini langu ni kwamba shule zote kote Marekani zitaanza kutumia vipindi hivi ili kuimarisha POD. Hata kama tunaweza kuanza na mwezi wa Septemba -kufanya kipindi kimoja kwa kila siku mpaka Septemba 21- huo utakuwa ni mwanzo mwema."
Christyn Pope, Mwalimu, Shule ya Jumuia ya Chula Vista Charter, San Diego, CA, Marekani

Waungaji mkono

Tunashukuru kuungwa mkono kutoka:

Rasilimali ya Elimu ya Marekani ya Peace One Day inasambazwa kwa ushirikiano na 

 

Asante pia kwa kutuunga mkono kutoka:

Salesforce.com foundationDHLFujitsuEcoverCofraVirgin UniteBen and Jerry's