Menu

Photographer: Vianney La Caer

 

ASANTE GOMA, DRC NA ULIMWENGU!

Mahali: Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Goma

Siku ya Amani, Jumapili Septemba 21, 2014

Tafrija ya Peace One Day iliongozwa na Akon Msanii Anayerekodi na Aliyeteuliwa katika tuzo za Grammy mara 5

Peace One Day iliweka historia mnamo mwaka 2014 kwa kuuteka Uwanja wa Ndege wa Goma_kwa uzuri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuandaa tafrija kuu iliyoongozwa na Akon msanii anayerekodi na aliyeteuliwa katika Tuzo za Grammy mara 5. Katika hali ya kihistoria, uwanja huu ndio uliofanyiwa hafla hii kuu iliyounganisha zaidi ya watu 50,000 wakisherehekea tumaini la amani kwenye Siku ya Amani, Septemba 21.

Namshukuru sana Rais Kabila kwa kuruhusu sherehe ya Peace One Day ya mnamo 2014 kuweza kufanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Goma. Hakukuwa na mahali pengine bora zaidi pa onyesho letu. Kwa yeye kufanya hivi, ujumbe thabiti na mkuu utatumwa ulimwenguni kwamba kuna hadithi nzuri zinazofanyika mahali hapa. Onyesho na wasilisho la Akon kwenye siku hii litakuwa ishara ya sura mpya ya tumaini katika kizazi cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na eneo la Maziwa Makuu. Shukrani zangu za dhati zimwendee Howard G. Buffet kwa kufadhili onyesho ili na Martin Kobler wa MONUSCO kwa kuweza kumfikia Rais Kabila ili kupata kibali cha sisi kuweza kuandaa onyesho katika uwanja wa ndege. Hii itakuwa ni sherehe ya kukumbukwa.

Jeremy Gilley

We would like to thank the  for making this concert possible.

 

With the support of the Government of the DRC and 

 

Kampeni ya Amani Katika Maziwa Makuu

Sherehe hii ndiyo kitovu cha ufahamisho kwa umma kuhusu kampeni ya miaka-3 ya Peace One Day nchini DRC na eneo la Maziwa Makuu barani Afrika.

Pata kujua zaidi kuhusu kampeni hii hapa:

 

Kufunguliwa Rasmi na...
Na Maonyesho Mengine Kutoka Kwa...

"Wakfu wetu umewekeza jumla ya dola milioni $175 katika DRC mashariki na katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika kwa imani kwamba watu wanahitaji fursa bora zaidi za kiuchumi za kufikia amani ya kudumu. Tuna furaha kwamba msaada wetu wa dola milioni $10 kwa Peace One Day utawawezesha kulenga kampeni yao katika eneo hili kwa miaka mitatu ijayo. Habari hizi za uwanja wa ndege kuwa ndio mahali ambapo itafanyika tafrija ya Peace One Day ya mwaka 2014 ni motisha mkubwa katika dhana ya  ufahamisho wa umma katika kampeni hii.

Howard G. Buffett

Nina furaha kwamba sherehe ya Peace One Day itakuwa Goma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa. Peace One Day inaweza kutegemea msaada kamilifu wa MONUSCO katika kuwezesha hili kufanyika. Namshukuru Rahis Kabila kwa kuruhusu matumizi ya uwanja huu wa ndege kuwa mahali ambapo tafrija ya Peace One Day itafanyika. Hii itakuwa siku ya kukumbukwa kwa watu wa Goma na eneon ili lote kwa ujumla.

Martin Kobler