Menu
Kumbukia Tafrija
Katika Mtazamo: Video za Sherehe za 2013

Tazama filamu mbili fupi hapo chini kuhusu utangazaji wa masaa 24 wa ulimwenguni kote na tafrija ya sherehe ya 2013 mjini The Hague

Peace One Day Inakuletea: Sherehe za Peace One Day za 2013 Mjini The Hague

Peace One Day ilizifanya sherehe zake za mwaka 2013 mjini The Hague ili kuadhimisha miaka mia moja ya Peace Palace.

Tafrija hii ya kihistoria mbele ya Peace Palace mjini The Hague ilijumuisha sehemu ya Utangazaji wa masaa 24 Ulimwenguni kote katia Siku ya Amani ya mnamo Jumamosi Septemba 21 mwaka 2013. Tangu kuanzishwa kwake, Peace Palace imekuwa ishara ya Amani na Haki ulimwenguni kote, ndipo pia pale ambapo Mahakama ya Haki ya Kimataifa, Mahakama ya Kudumu ya Upatanisho (Permanent Court of Arbitration), na Maktaba sifika ya Peace Palace ilipo.

Ilikuwa ni heshima kubwa kufanyia Sherehe za 2013 katika mahali kama hapa pa kihistoria. Hafla yenyewe ilikuwa na maonyesho kutoka kwa wasanii wasifika wa kimataifa na michango isiyokuwa ya kawaida kutoka ulimwenguni kote, kuangazia ufahamisho wa siku na kujenga kushiriki kutoka kwa watu binafsi na mashirika katika kila bara.

Jiunge nasi katika Facebook na mfuate Jeremy katika Twitter kwa habari za hivi punde na uanze kufikiria kuhusu nani utakayeridhia naye amani mnamo Jumapili Septemba 21 mwaka 2014 katika Siku ya Amani.

Ikiwemo Michango Kutoka Kwa:

   

Moja Kwa Moja Kutoka Kwa Medellín

Sherehe za Peace One Day Nchini Kolombia 2013

Jiji la Medellín ndilo ambalo tafrija ya Siku ya Amani kwa mwaka wa tatu mfululizo ilifanyiwa. Mwaka 2013 ndio uliokuwa mwaka mkubwa zaidi katika sherehe hizi za Siku ya Amani ya Medellín, kwani watu watajika na waheshimiwa katika jumuia ya Kolombia walikuwepo, pamoja na utangazwaji wa tafrija hii moja kwa moja ikiwa ndiyo sehemu ya hali ya mtandaoni ya masaa 24 ya Peace One Day kwenye mtandao kupitia Youtube Live katika Siku ya Amani.

Tafrija hii ilikuwa na uigizaji kutoka kwa: Xoel López(Hispania), Andrés Gualdrón (Kolombia), Rialengo (Kosta Rika), C15 (Kolombia) na César López (Kolombia).

Uonyeshwaji wa filamu ya hali halisi: Safari ya Peace One Day

“Kila ninaposimama mbele ya kundi la watu, wawe wawili au elfu mbili, huwa nawaelezea hadithi ya Peace One Day, maendeleo ya Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21 na pale ambapo twaelekea. Mimi huwaambia kuhusu kampeni zote tofauti ninazokuwa nazo na ukuzi usiokuwa wa kawaida katika ufahamisho na uhusishwaji wa watu na mashirika katika siku hii ulimwenguni kote. Mimi hufanya hivi ili watu waweze kuelewa kuwa ndani ya kipindi kifupi sana cha muda namna ambavyo kurasmisha Siku ya Amani ni mchakato tu. Nafanya hivyo ili watu waweze kuelewa kwamba ufanisi wa Siku ya Amani unatokana na watu binafsi wanaojihusisha na wanaomiliki siku hii. Na hivyo ndivyo ninavyotaka kufanya kupitia katika filamu hii ya hali halisi ya hivi punde zaidi kusimulia hadithi rahisi na kuwapatia moyo watu kuchukua uongozi.” Jeremy Gilley, London, Julai 2013

Vipindi Vya Moja Kwa Moja Ulimwenguni Kote

Peace One Day iliwaleta pamoja washiriki wake ili kusherehekea Siku ya Amani ya mnamo Septemba 21, kwa kushiriki katika vipindi vya Moja kwa moja Ulimwenguni kotekupitia katika jukwaa la Youtube Live, ili kuwatia moyo na kuwawezesha watu ulimwenguni ili waje pamoja na kuwa kitu kimoja kwenye siku hiyo.

Hii ilikuwa ni midahalo ya mtandaoni iliyodumu kwa takribani dakika 30 katika kila mdahalo. Watu muhimu wakiwakilisha mabara yote ya ulimwengu, kutoka kwenye sekta tofauti za jumuia, walishiriki, wakiwemo waigizaji, wanamuziki, wasanii, wajumbe wa kiwango cha juu wa Umoja wa Mataifa au serikali na wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na yale ya kati ya serikali mbalimbali. Mtandao wa kijamii ndio uliokuwa mwendeshaji mkuu katika uonekanaji wa kiwango cha juu kwa yote, kwani, Peace One Day ilizindua mtandao yake yenyewe na ile ya washirika wake katika sekta zote pamoja na jumuia za mtandaoni za washiriki wenyewe.

Idadi ya watu kutoka duniani kote iliweza kutazama Vipindi vya Moja kwa moja Ulimwenguni kote, kama sehemu ya Utangazaji wa masaa 24 Ulimwenguni kote kwenye YouTube.

Zingatio la kuuliza maswali lilikuwa katika Siku ya Amani, ya mnamo Septemba 21 na mada ya Peace One Day ‘Nani utakayeridhia naye amani?’

Ili kuona pale ambapo washiriki wanatokea bofya hapa:

Chukua Hatua Kwa Ajili ya Amani

Misururu ya mahojiaono na baadhi ya waigizaji sifika, wakizungumzia kuhusu amani na mada ya Siku ya Amani: ‘Nani utakayeridhia naye amani?’

Kila mahojiano yalijumuisha hotuba iliyochaguliwa na kuwasilishwa na muigizaji, inayohusiana na amani.

Waigizaji walioshiriki walijumuisha na:

Wimbo Kwa Ajili ya Amani

Wakati wa kipindi cha muda wa masaa 24 kulikuwa na video za muziki zilioundwa maalum kwa maonyesho ya moja kwa moja kutoka kwenye tafrija za awali za Peace One Day, pamoja na mahojiano na kila msanii.

Wanamuziki waliochangia walijumuisha: