Menu
  • العربية العربية
  • 繁體中文 繁體中文
  • English English
  • Français Français
  • Português Português
  • Русский Русский
  • Español Español
  • Kiswahili Kiswahili
Mahojiano ya Monako

MAONYESHO KUTOKA KWA: JESSIE J

Msanii huyu wa kimataifa anayerekodi Jessie J amethibitisha maonyesho yake katika hafla ya tamasha la Peace One Day nchini Monako mnamo Alhamisi tarehe 22 Mei. Msanii huyu aliyezaliwa London, ambaye ameuza zaidi ya rekodi milioni 12 na ameweza kufanikiwa kupata tuzo za muziki bora kimataifa katika kiwanda hiki, atatumbuiza katika hafla ya Peace One Day katika eneo la Salles des Etoiles ili kuonyesha msaada wake katika vuguvugu hili la Peace One Day. 

Mnamo Alhamisi Mei 22 mwaka 2014 Peace One Day Itakuwa na furaha ya kuwa mwenyeji wa mapokezi ya vinywaji na vitafunio pamoja na milo ya usiku mitatu katika tamasha litakalofanyika katika eneo sifika la Salle des Etoiles, Monako.

Kukuza ufahamisho wa kampeni ya Peace One Day katika DRC na Eneo la Maziwa Makuu la Afrika kwa ajili ya Siku ya Amani, itakayofanyika mnamo Septemba 21, mlo huu wa usiku katika tamasha utaandamana na muziki wa moja kwa moja kutoka kwake msanii Jessie J pamoja na mnada wa formula 1 memorabilia na kazi ya sanaa kutoka kwa wasanii wa kisasa wanaongoza Uingereza.

Ili kuona picha kutoka katika kampeni hadi kufikia sasa, tafadhali bofya kitufe kilicho upande wa kulia.

Peace One Day inayo heshima kuu kutokana na hafla hii ambayo imeihudhuriwa na kinara  mkuu H.S.H. Mwana mfalme Albert II wa Monako, pamoja na kushiriki kwa wageni wengine wa vyeo vya juu wakiwa ni wanachama wa kundi la Lotus F1.

Kipindi cha jioni kitaweza kujumuisha michango kutoka kwake Balozi wa Peace One Day na mwigizaji aliyeteuliwa mara mbili katika tuzo ya akademia Jude Law.

 

Je, Mnada wa Peace One Day utafanywa mnamo tarehe Mei 22?

Angalia maelezo zaidi hapa chini:

 

Umeungwa mkono na:

 

Kwa taarifa zaidi zikiwemo maelezo ya tiketi na mahali pa kukaa, tafadhali bofya hapa chini:

Peace One Day itakuwa na furaha kubwa endapo utajiunga nasi.

 

Tafadhali tuma fomu zako za kujiandikisha zilizojazwa kwa:

Corporate.team@peaceoneday.org

 

Kwa fursa za ufadhili tafadhali wasiliana na:

David.henry@peaceoneday.org

Hafla hii inafanywa ili kuisaidia idara ya Elimu ya Peace One Day na vilevile kukuza ufahamisho wa mradi wa amani wa Peace One Day katika nchi ya DRC na Eneo la Maziwa Makuu. Pata kujua zaidi hapa chini: